Winga wa klabu ya Simba Sc Joshua Mutale ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya kalenda ya Fifa.
Mutale amerejea baada ya muda mrefu kukosekana kutokana na kutopata nafasi katika klabu yake ya Simba Sc na hivyo kukosa nafasi pia katika timu ya Taifa hilo.
Zambia itacheza na Sudan na Tunisia katika ratiba ya michezo ya kirafiki ya kalenda ya Fifa ambapo kocha Avram Grant ameita mastaa takribani 25 katika kikosi hicho.
Mbali na Mutale pia mastaa wa Yanga Sc Kennedy Musonda na Clatous Chama nao wameitwa kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya FIFA dhidi ya Sudan na Tunisia.