Klabu ya Yanga sc ilianzishwa rasmi mwaka 1935 ikiwa kama klabu ya wanachama iliyokua na lengo la kujumuisha vijana wa kitanzania katika kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii lakini ilianzia kama timu ya New Youngs ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.
Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs vijana wa Dar es Salaam walikuwa na desturi ya kukutana viwanja wa jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani Boys na Ndani ya kipindi kifupi timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo, miongoni mwao waliovutiwa na uanachama wa klabu hiyo ni Tabu Mangala (Sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926 walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi sasa kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo bandarini.
Baada ya mkutano huo, timu ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika na kusababisha timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana wa Jangwani hao.
Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wanatembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani wao, kwamba katika kipindi hicho wao ndiyo zaidi, kwa sababu Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Italiana.
Taliana FC ilipata mafanikio ya halaka na haikushangaza ilipopanda ligi Daraja la pili kanda ya Dar es Salaam kisha mwanzoni mwa miaka ya 1930 Taliana waliamua kuachana nalo mapema kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.
Kila kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu vipya pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs waliweza kutwaa kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.
Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland ambapo Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.
UMILIKI WAKE
Kwa msingi wa historia hapo juu ambapo timu hiyo kwa mara ya kwanza ilipitisha katiba yake ya mwaka 1968 ambapo ilisema kuwa timu hiyo ni timu ya wanachama kwa asilimia mia moja lakini katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2011 na 2021 ambapo kwa sasa timu hiyo inamilikiwa na wanachama kwa 49% huku 51% zikienda kwa mwekezaji ambaye mpaka sasa taratibu zinaendelea ili kuanza kutumia mfumo mpya.
MUUNDO WA UONGOZI NDANI YA KLABU HIYO.
Muundo wa uongozi kwa mujibu wa mabadiliko mapya ya katiba mwaka 2021 klabu hiyo sasa inaongozwa na Rais ambaye ni Eng.Hers said huku msimamizi wa shughuli za kila siku akiwa ni Afisa mtendaji mkuu wa klabu ambaye kwa sasa ni Andre Mtine sambamba na bodi ya wakurugenzi wa klabu ambao wenyewe wanahusika Zaidi na kufanya maamuzi ya klabu ambao kwa sasa inajumuisha majina kama Alex Ngai,Muniry Said,Eng.Hersi Said,Anthony Mavunde,Rodgers Gumbo na Mh.Abbas Gulamali ambao kwa pamoja ndio hutoa maamuzi kwa klabu hiyo.
BARAZA LA WADHAMINI.
Hiki ndicho chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya klabu hiyo ambacho huundwa na wajumbe watano wakiongozwa na Mama Fatma Karume,Mh.Kapteni George Mkuchika,Mh.Mwigulu Nchemba,Mh.Geofrey Mwambe na Abbas Tarimba ambapo hawa hutoa ushauri kwa kamati tendaji ya klabu hiyo kuhusu mambo mbalimbali.
UDHAMINI.
Klabu hiyo pamoja na kuwa na vyanzo vingine vya fedha kama mapato ya mlangoni,michango ya wanachama na mapato kupitia mitandao ya kijamii,pia klabu hiyo ina wadhamini mbalimbali akiwemo mdhamini mkuu kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportspesa na wadhamini wengine kama Hier,Azamtv,Karimjee Group,kampuni ya Gsm kupitia vinywaji vyake na wengine.
UFADHILI
Tangu msimu wa 2019-2020 boss wa Gsm Ghalib Said Mohamed alianza kuisaidia klabu hiyo taratibu na hatimaye kuongeza misaada maradufu akisaidia fedha za usajili na kusaidia kulipa posho mbalimbali klabuni hapo zilizoipa nguvu klabu hiyo kiuchumi na kusaidia kuipa nguvu uwanjani na hatimaye sasa imechukua ligi kuu na kombe la shirikisho mara nne mfululizo mpaka sasa.