Site icon Sports Leo

Mwamnyeto Arejea Yanga sc

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Sc Ali Kamwe ameweka wazi kuwa nahodha wa klabu hiyo Bakari Mwamnyeto tayari amerejea kikosini humo baada ya kukosekana katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya pili dhidi ya Al Merrekh ya nchini Sudan.

Nahodha huyo alikosa mchezo huo kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia na sasa tayari ameungana na wenzake kambini tayari kwa kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika siku ya Jumatano katika uwanja wa Azam Complex chamazi jijini Dar es salaam.

“Leo kambi imeanza kwaajili ya mchezo dhidi ya Namungo siku ya jumatano saa moja usiku huku pia nahodha Mwamnyeto amerejea akitokea kwenye matatizo ya kifamilia na atakuwa sehemu ya wachezaji.Alisema Kamwe

“Msimamo wa ligi kuu hauwezi kutazamika kama Yanga hawako juu, huwa hauwezi kuwa msimamo wa ligi kuu,Tulisafiri kwenye majukumu ya kimataifa watoto wakaja juu lakini tunakwenda kurejea katika kilele cha msimamo”.

“Mchezo wa jumatano dhidi ya Namungo Fc utakuwa mchezo mkubwa kwa sababu Namungo wana kikosi kizuri na wana mwalimu mzuri ambaye pia alikuwa katika kikosi chetu msimu uliopita.”

Katika Mkutano uliofanyika leo, Septemba 18, 2023 na Waandishi wa Habari Kamwe pia amesema kuhusu viingilio vya kushuhudia mtanange kati ya Yanga na Namungo mchezo wa Ligi Kuu ya NBC itakuwa ni VIP A  Tsh 20,000 na VIP B Tsh 10,000 huku Mzunguko ukiwa ni Tsh 5,000.

Klabu hiyo sasa itarejea katika michezo ya ligi kuu nchini baada ya awali kusimama kutokana na kuwa na majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania huku pia ikiwa na michezo ya kimataifa ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Katika ligi kuu timu hiyo imecheza michezo miwili dhidi ya JKT Tanzania na Kmc na zote iliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Exit mobile version