Home Makala Mwenda Amalizana na Simba sc

Mwenda Amalizana na Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Beki Israel Mwenda amemalizana na Klabu ya Simba Sc na sasa rasmi si mchezaji wa klabu hiyo baada ya kurejesha pesa zote alizochukua kama dau la usajili msimu huu.

Mchezaji huyo alisaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia Simba sc ambapo baada ya muda aliamua kutafuta timu nyingine ili kuondoka klabuni hapo na Viongozi wa Klabu hiyo walikua tayari kumuachia kwa sharti la kurudisha pesa ya kusainia mkataba ambayo alikua amelipwa yote kwa mkupuo.

Tayari mchezaji huyo ameshakubaliana maslahi na Singida Big Stars ambao wamelipia pesa hizo kwa Simba sc na tayari mchezaji huyo ameshasaini mkataba na Klabu hiyo akienda kuchukua nafasi ya Kelvin Kijiri ambaye amejiunga na Simba sc.

banner

Sababu kubwa ya beki huyo kuachana na Simba sc inatajwa kuwa ni kutokana na maelewano hafifu baina yake na Shomari Kapombe ambaye wanacheza eneo moja la beki wa kulia.

Mwenda alijiunga na Simba sc msimu wa 2021 akitokea klabu ya Alliance Fc akienda kusaidia na Kapombe eneo la beki wa kulia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited