Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc Clement Mzize amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu kwa mwezi Disemba akiwashinda Prince Dube wa Yanga sc na Feisal Salum wa Azam Fc.
Mzize katika mechi nne alizoichezea Yanga sc amefunga goli nne na kuhusika kwenye magoli matatu ambapo kwa ujumla akiwa amehusika katika magoli saba na kuisaidia klabu yake kupaa kutoka nafasi ya tatu hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu.
Hivyo hivyo kocha mkuu wa Yanga Sc Sead Ramovic, amechaguliwa kuwa kocha bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Desemba ambapo amewashinda Kocha Rachis Taoussi wa Azam Fc na Fadlu Davis wa Simba sc, alioingia nao fainali.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ramovic katika michezo minne aliiongoza Yanga sc katika michezo minne na kupata ushindi katika michezo yote huku akifunga magoli 16 na kufungwa mawili.