Timu ya Namungo iliyovunja rekodi ya Tanzania Prisons kwa kuwapa kichapo cha mabao 3-2 kwenye mchezo wa ligi imejiandaa kuwapa dozi Mbao Fc kwenye mchezo ujao wa ligi kuu nchini.
Kocha mkuu wa Namungo Hitimana Thiery alisema kuwa watakuwa na mchezo kwanza wa kombe la FA na Biashara United kisha zamu ya Mbao Fc na Alliance Fc itafata katika uwanja wao wa nyumbani hivyo wanaahidi kufanya vizuri ili kupata matokeo mazuri.
Namungo itapambana na Mbao Fc katika uwanja wa Majaliwa siku ya Jumamosi 1 Februari,2020.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.