Mshambuliaji Reliants Lusajo ameifungia mabao 2 klabu ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union katika ushindi wa 3-1 mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na washambuliaji Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 38 na mzawa, Reliant Lusajo mawili dakika ya 81 na 85, wakati bao pekee la Coastal alijifunga Abdulmik Zacharia dakika ya 46.
Namungo inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya sita, ikiishushia Coastal nafasi ya saba ambayo inabaki a pointi zake 17 za mechi 13 pia.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Huu ni mchezo wa pili kwa Coastal Union kupoteza mchezo wa ligi kuu baada ya kufungwa na Yanga sc kwa mabao 2-0 huku kukiwa na mgawanyiko katika uongozi wa klabu hiyo.