Kiungo Issah Ndala anaweza kutemwa katika kikosi cha Azam Fc ili kumpisha kiungo Yannick Bangala ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Yanga sc baada ya kukamilisha usajili mapema hivi leo.
Ndala inasemekana kuwa sio chaguo la kocha wa Azam Fc Yousouph Dabo na ndio maana aliwaruhusu viongozi kumsajili Bangala baada ya kumuona katika mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho uliofanyika jijini Tanga mwezi juni mwaka huu.
Bangala ambaye ni mchezaji bora wa ligi kuu nchini msimu wa 2021/2022 alianza kuwekwa benchi na kocha Nasredine Nabi ambaye alianza kumtumia zaidi Khalid Aucho sehemu ya kiungo cha chini.
Azam Fc ilimsajili Ndala baada ya kumuona katika mchezo wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Plateau Fc ya nchini Nigeria.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Azam Fc inalazimika kumchomoa Ndala katika usajili wao ili kutimiza idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu nchini.