Home Makala Ndemla Asaini Singida Big Stars

Ndemla Asaini Singida Big Stars

by Sports Leo
0 comments

Aliyekua kiungo wa klabu ya Simba sc Said Ndemla ambaye alimalizia msimu akiitumikia klabu ya Mtibwa Sugar kwa mkopo inasemekana tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya Singida Big Stars ambayo imepanda ligi kuu msimu ujao.

Timu hiyo ambayo zamani ilijulikana kama Dtb imemsainisha kiungo huyo wa ushambuliaji mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru akiwa amemaliza mkataba wake wa miaka miwili katika klabu ya Simba sc ambayo ilimtoa kwa mkopo kwenda Mtibwa sugar kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Azam Fc inatajwa nayo ilikua na mpango wa kumsajili mchezaji huyo lakini kwa taarifa hizi inaonekana Azam Fc imezidiwa kete na Singida Big Stars katika kumsainisha mkataba staa huyo ambaye amekulia Simba sc akianza kuichezea tangu katika kikosi cha vijana kilichotikisa miaka hiyo kikiwa na vijana kama Jonas Mkude,Ramadhani Singano na wengineo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited