Raia wa Brazil ,Willian Borges da Silva ambaye ni mchezaji katika timu ya Chelsea amewaomba mabosi wake ruhusa ya kuondoka London na kuifuata familia yake nchini Brazil.
Da Silva mwenye miaka 31 amesema kwa sasa ameikumbuka familia yake , hali ya kuwa mpweke muda mrefu imemchosha jambo linalomfanya aikumbuke familia yake.
“Nimekaa mbali na familia kwa muda mrefu, mimi nipo London kwa sasa familia yangu ipo Brazil nahitaji kwenda kuiona na kuwa karibu nao hali ya upweke inaumiza,” alisema Willian
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.