Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Nuno Espirito Santo amesema kuwa nahodha ya timu hiyo Harry Kane bado ni mchezaji wao kwasasa na atamsubiri wazungumze atakaporejea.
Mchezaji huyo yupo katika mapumziko ya likizo baada ya kuiongoza England katika fainali za michuano ya Euro 2020.
Mchezaji huyo anaamini kuwa ana makubaliano ya mdomo ya kiungwana na mtendaji wa timu hiyo Daniel Levy kuruhusiwa kuondoka na ameweka wazi nia yake ya kuondoka katoka dirisha hili, akihusishwa zaidi kuhamia kwa mabingwa wa England Manchester City.
Nuno aliongeza ”ninamtakia mapumziko mazuri,ili atakaporejea aone ni jinsi gani kila mmoja wetu anavyojitolea ilimtuwe bora.
”Sisi ni watu wenye ndoto na mipango thabiti,tunataka kufanya vema na tunamtegemea kwa sababu ni mchezaji bora wa daraja la dunia”.