Beki wa kati wa Tanzania Abdallah Shaibu Ninja anatakiwa kutua nchini Latvia tarehe 15 ,Februari kwaajili ya kufanya vipimo katika klabu ya FK Rigas Footbola Scola inayoshiriki ligi kuu nchini humo na iwapo atafuzu atasaini mkataba usiopungua mwaka mmoja.
Kabla ya kuanza safari ya FK Rigas Footbola Scola ,Ninja alikuwa amesajiliwa timu ya MFK Vyskov ya jamhuri ya Zcech kwa miaka minne ila hakuweza kuitumikia timu hiyo kwani alichukuliwa kwa mkopo na timu inayoshiriki ligi kuu Marekani La Galaxy.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Fk Rigas ,Aleksandrs Usovs alituma kadi ya mualiko kwa mchezaji huyo na kumpa ofa ya kumgharamikia mahitaji yote muhimu atakayohitaji hadi ukamilisho wa vipimo utakapo kamilika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.