Home Makala Oezil Kutemwa Arsenal Msimu Huu

Oezil Kutemwa Arsenal Msimu Huu

by Sports Leo
0 comments

Tetesi zinaeleza kuwa Mesut Oezil ambaye ni mzaliwa wa Uturuki na raia wa Ujerumani hajajumuishwa kwenye kikosi cha wanasoka 25 kinachotegemewa na Arsenal kwenye kampeni za Europa League msimu huu wa 2020/2021.

Kuachwa nje kwa Oezil katika kikosi kilicho chini ya kocha mkuu,Mikel Arteta ambacho kitashiriki soka ya Europa League kunaashiria kwamba huenda akawa amechezea Arsenal mchuano wake wa mwisho licha ya kwamba bado ana miezi minane Emirates.

Arteta aliamua kumtema Oezil kikosini baada ya kushindwa kumlipa mwanasoka huyo dau kubwa ambalo anastahili kupokea kulingana na mkataba wake ili atafute hifadhi mpya kwingine.

banner

Oezil kwasasa ana uhuru wa kuvunja ghafla mkataba wake na Arsenal na kuingia katika sajili mpya ya kikoi chochote kisichokuwa cha EPL kabla ya Octoba 19,2020.

Pia anaweza kuwapa mabosi hao wa Emirates barua ya kumruhusu ajiunge na klabu yoyote nyingine barani Ulaya katika muhula mfupi wa uhamisho wa wachezaji mnamo Januari 2021.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited