Home Makala Opah Atua Uturuki

Opah Atua Uturuki

by Sports Leo
0 comments

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Simba Queens, Opah Clement jana Jumatano (Machi 08) alitarajiwa kutambulishwa rasmi kwa Mashabiki wa Klabu ya Beskitas inayoshiriki Ligi Kuu Uturuki.

Opah aliondoka nchini juzi Jumanne (Machi 07) majira ya Alfajiri na kwenda moja kwa moja Uturuki kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la kujiunga na klabu hiyo.

Opah hadi anaondoka nchini alikuwa anaitumikia Klabu ya Simba Queens na ameondoka akiwa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Wanawake akiwa nayo tisa.

banner

Meneja wa Simba Queens, Seleman Makanya amesema kuwa: “Opah huenda akatambulishwa leo (jana) kwa sababu juzi aliondoka asubuhi na ilitarajiwa mchana awe ameingia.”

Opah, amejiunga na Beskitas kwa mkataba wa miaka miwili, Hii inakuwa mara ya pili kwa Opah kwenda Uturuki kucheza soka, mwaka jana alilijunga na Yikatel Kayseri kwa mkataba wa muda mfupi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited