Home Makala Pogba Arejea Mazoezini

Pogba Arejea Mazoezini

by Dennis Msotwa
0 comments

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amerejea katika mazoezi  baada ya kuwa nje kutokana na kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Pogba ana uwezekano mkubwa wa kutocheza mchezo wa kwanza ndani ya Premier Septemba 19 ambapo klabu yake ya Man United itavaana na Crystal Palace kwenye uwanja wa Old Trafford.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa,kurejea kwa Pogba kwenye mazoezi hakumpi asilimia 100 kuwa atashiriki mechi ya kwanza kwani hayupo kwenye sehemu ya kikosi ambacho kinaendelea na mazoezi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited