Arsenal wamepanga kumwadhibu vikali mshambuliaji, Alexandre Lacazette baada ya kupata ripoti kuwa nyota huyo ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa alipatikana akivuta gesi ya Nitrous Oxide maarufu kama ‘Laughing Gas’ iliyokuwa imejazwa ndani ya puto .
Gazeti la Daily Star nchini Uingereza lilichapishwa makala zenye picha zilizoonyesha Lacazette akiwa na puto yenye gesi hiyo mdomoni.
Ni wiki moja pekee imepita tangu Lacazette apatikane miongoni mwa wanasoka wengine wa Arsenal waliokiuka kanuni mpya za afya zinazodhibiti maambukizi dhidi ya virusi vya corona.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Lacazette pia alionekana akiwa karibu sana na mwanamume mmoja aliyekuwa akimwoshea gari lake jijini London, Uingereza na kuvunja kanuni inayotaka mtu kudumisha umbali wa hadi mita mbili kati yake na mwingine .