69
Tajiri namba tisa barani Africa,Patrice Motsepe amechaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la soka barani Africa-CAF katika uchaguzi uliofanyika leo mjini Rabat-Morocco.
Motsepe mwenye umri wa miaka 59 amechaguliwa kufuatia washindani wake watatu kujitoa wiki iliyopita huku aliyekuwa rais wa CAF tangu mwaka 2017 Ahmad Ahmad adhabu yake ya kufungiwa kujihusisha na michezo ikipunguzwa kutoka miaka 5-2 hivyo kukosa sifa ya kugombea Urais wa CAF.
Washindani waliojitoa wiki iliyopita ni Jacques Anouma,Ahmed Yahya na Augustin Senghor.
Mostepe ni ndugu wa rais wa Afrika Kusini,Cyril Ramaphosa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.