Wachezaji wa klabu ya Wydad Casablanca watapata karibu $ 4,500 [zaidi ya Sh mil 10] KILA MMOJA ikiwa watashinda mechi yao dhidi ya wapinzani wao wakubwa Raja Casablanca katika Casablanca Derby Jumapili hii ya tarehe 21 Machi 2021 huko kwenye Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola Pro.
Mechi hiyo ya wapinzani wa jadi inatajwa kuwa na mvuto nchini humo na barani Afrika huku watu wengi nchini Tanzania wakifuatilia kutokana na uwepo wa staa huyo.