Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuachana na staa Sergio Ramos baada ya kudumu klabuni hapo kwa miaka 16 baada ya kushindwa kuafikiana kuhusu mkataba mpya licha ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kumhitaji.
Ramos aliyejiunga na klabu hiyo mwaka 2015 akitokea Sevilla ameichezea klabu hiyo jumla ya michezo 670 huku akishinda ubingwa wa Laliga mara tano na klabu bingwa barani ulaya mara nne.
Kocha Carlo Ancelloti ameonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo huku klabu hiyo ikiwa tayari kumpa mkataba mpya ikiwa atakubali kupunguza kiwango cha mshahara anaolipwa hivi sasa huku mkataba wake ukiwa unaelekea ukingoni mwezi juni na anatarajia kutangaza mahali atakapoeleke hivi punde.