Home Makala Real Madrid Kuanza Mazoezi Valdebebas

Real Madrid Kuanza Mazoezi Valdebebas

by Sports Leo
0 comments

Wachezaji wa Real Madrid wanatazamiwa kuanza mazoezi Mei 11 mwaka huu ambapo yatakuwa mazoezi binfasi yatafanyika chini ya uangalizi maalum huku yakiwa ni wachezaji na makocha wachache.

Wachezaji mbalimbali wa La Liga wanatarajiwa kupimwa afya zao wiki ijayo kuonekana kama hawana maambukizi ya corona na kuhakikisha kila mmoja anakuwa salama kuanzia wachezaji hadi makocha kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja na kucheza michezo ya La Liga.

Real Madrid watafanya mazoezi yao rasmi siku hiyo ya Jumatatu ya 11 Mai, kwenye viwanja vyao vya mazoezi vijulikanavyo kama Valdebebas.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited