Mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amefikisha idadi ya magoli 98 katika timu yake ya taifa pamoja na hat-trick 9 katika timu hiyo.
Nyota huyo jana usiku alifunga magoli matatu katika ushindi wa 6-0 dhidi ya timu ya taifa ya Lithuania, katika mchezo wa kundi B kufuzu michuano ya Euro.
Hii ni hat-trick ya 55 katika maisha yake ya soka huku akiwa ameichezea Ureno jumla ya mechi 37 na kufunga mabao 38 tangu afikishe miaka 31 huku akifunga mabao 55 katika michezo 123 hapo kabla.