103
Nyota wa klabu ya manchester united, Cristiano Ronaldo (37), hii leo amerejea mazoezini pamoja na Wachezaji wenzake katika kikosi cha kwanza baada ya kuondolewa kwa muda kwenye kikosi hicho kutokana na utovu wa nidhamu.
Baada kuejea katika mazoezi ya klabu hiyo Ronaldo anatarajiwa kwanza kufanya mazungumzo na kocha wake Erik Ten Hag kisha atajiunga na nyota wenzake kujiandaa mchezo wa Europa League ambapo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na Sheriff Tiraspol katika mchezo ujao w utakaopigwa katika dimba la Old Trafford Alhamis hii.
Ronaldo alizuiwa kufanya mazoezi na kikosi cha wakubwa na kocha Eric Ten Hag baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya Tottenham Hotspurs ambapo aliondoka dakika ya 89 ya mchezo baada ya kukataa kufanyiwa mabadiliko akidai kuwa muda ulikua umekwisha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.