Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amesaini rasmi kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia mashetani wekundu Manchester United hadi mwaka 2023.
Ronaldo amekamilisha vipimo vya afya huko Lisbon Ureno na ameweka saini mkatanba wake kupitia wakala wake Jorge Mendez.
Klabu ya Manchester United kwasasa inashughulikia maswala ya Visa ili mshambuliaji huyo aweze kupatikana kucheza mechi dhidi ya Newcastle United tarehe 11 Septemba katika dimba la Old Trafford.Vipengele vingine vyote vya mkataba wake vimeshakamilishwa na bodi ya klabu yake hiyo mpya.
Mshahara wa mshindi huyo mara 5 wa Balon D’or utakuwa ukiongezeka kulingana na vipengele vilivyojumuishwa katika mkataba wake ambavyo vinategemea zaidi mafanikio binafsi na yale atakayoleta katika timu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Cristiano aliondoka Man Utd mwaka 2009 na kutimkia Real Madrid,akiwa Manchester mchezaji huyo alitwaa mataji matatu ya Epl,klabu bingwa Ulaya mara moja,klabu bingwa dunia mara moja pamoja na tuzo ya moja ya Balon D’or aliyoitwaa mwaka 2008.
Kurejea kwa Ronaldo Old Trafford kunatajwa kuwa ni ushawishi wa Sir Alex Ferguson ambaye anachukuliwa kama baba na mchezaji huyo ktokana na kuongea moja kwa moja na mama mzazi wa Ronaldo juu ya kutakiwa tena kwa kijana huyo na miamba hiyo ya England.Pia inasemekana wachezaji wenzake wa zamani walifanya kazi kubwa kuongea na mchezaji huyo kumshawishi arejee tena na imekiuwa furaha kubwa sana kwao kwa hilo kufanikiwa.