Nyota wa Juventus Christian Ronaldo mwenye umri wa miaka 35 amefikisha jumla ya mabao 50 akiwa kwenye maisha ya soka nchini Italia siku ya Jumapili ambapo ilikuwa ikichuana na Fiorentina ambapo timu yake ilishinda mabao 3-0.
Christian Ronaldo amefikisha mabao hayo 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 70 na kumfanya awe nafasi ya pili kwa watupiaji wenye mabao mengi ndani ya muda mfupi huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Icon wa AC Milan, Andriy Shevchenko aliyetupia mabao 50 baada ya kucheza mechi 69.
R9 Ronarldo, ambaye ni raia wa Brazili anakamata nafasi ya tatu kwa kufikisha mabao 50 kwenye mechi 77 akiwa Inter na majeraha ndio sababu ya kumchelewesha kufikisha mabao hayo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.