Home Makala Rooney Aimaliza Norwich Kwa Bao 1-0

Rooney Aimaliza Norwich Kwa Bao 1-0

by Sports Leo
0 comments

Wayne Rooney aliwapa Derby County ushindi wa bao 1-0 uliowavunia alama tatu za kwanza katika ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza(Championship) katika mchezo wa jana Octoba 3,2020.

Rooney alipiga mpira huo kutoka hatua ya 20 na kumwacha hoi kipa Tim Krul wa Norwich City dakika tatu kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa kipindi cha pili kupulizwa.

Norwich walisalia kujilaumu wenyewe katika mchuano huo ulioshuhudia fowadi Teemu Pukki akipoteza mkwaju wa penalti katika dakika ya 49 uwanjani Carrow Road kutokana na tukio la beki George Evans kunawa mpira alioelekezwa na kiungo Onel Hernandez.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited