Home Makala Ruvu Shooting Waipiga Kmc

Ruvu Shooting Waipiga Kmc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Ruvu Shooting imefanikiwa kufuzu raundi inayofata ya kombe la shirikisho baada ya kuifunga Kmc kwa ushindi wa matuta wa 7-6 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Mchezo huo uliotawaliwa na ufundi mwingi hasa eneo la katikati mwa uwanja lililomilikiwa vizuri na Kenny Ally wa Kmc ambapo dakika ya 24 Kmc walipa bao la uongozi likifungwa na Idd Kipagwile huku Ruvu Shooting wakisawazisha kupitia kwa Abrahiman Musa dakika ya 61 kwa faulo ambayo kipa wa Kmc Juma K. Juma hakuiona.

Mpira mpaka unamalizika dakika 90 za mchezo timu hizo zilikua zipo sare ya 1-1 na ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ilipoanza na penati tano za awali timu zote zilifunga mpaka zilipoanza zile za piga nikupige ndipo mchezaji wa Kmc alipokosa na kupelekea timu yake kutolewa katika michuano hiyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited