Msafara wa wachezaji,Benchi la ufundi na viongozi unatarajiwa kuelekea jijini Mbeya kesho katika kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City huku kiungo Saido Ntibazonkiza akishindwa kujumuishwa katika msafara hiyo.
Orodha ya mastaa wa klabu hiyo watakaosafiri imetangazwa huku Mburundi huyo akikosekana kutokana na kuwa majeruhi huku Dickson Job na Yacouba Sogne wakijumuishwa kutokana na kuimarika kwa afya zao.
AbdalaH Shaibu naye ana hatihati ya kukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na maralia huku usajili mpya Fiston akiwa miongoni mwa wasafiri kuelekea mchezo huo utakaochezwa tarehe 13 siku ya jumamosi,
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.