Nyota mpya wa Aston Villa Mbwana Samatta amewashukuru sana watanzania na watu wote waliokuwa wakimuombea mema aweze kupita katika usajili huo na ameahidi kuendelea kupambana kwani alipofikia ni suala la kumshukuru mungu.
Samatta mwenye miaka 27 alianza kucheza ndani ya Simba na kujinga Tp Mazembe aliibuka KRC Genk mwaka 2016 ambapo amefunga jumla ya mabao 76 kwenye mechi 191 ndani ya Genk na mabao 18 katika mechi 51 za timu ya Taifa ya Tanzania.
“Ninamshukuru Mungu kwa hatua niliyofikia kwa sasa ,sapoti ya mashabiki na maombi ya watanzania kiujumla yananifanya niwe hapa nilipo”alisema Samatta.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na utaratibu wa ligi kuu England kuwasilisha wachezaji kabla ya masaa 15 ya mchezo inamfanya Mbwana Samatta kutoweza kushiriki mechi ya leo dhidi ya Watford.