Mwanamama nguli katika mchezo wa tenisi Serena Williams amejiondoa katika mashindano ya Wimbledon baada ya kuumia katika mchezo wa mtoana dhidi ya Aliaksandra Sasnovich.
Williams aliteleza katika set ya tano ya mchezo na ilipofika set ya saba alishindwa kuendelea kutoana na maumivu makali ya nyama za paja’,hali iliyomsababishia kumwaga machozi.
Mashabiki waliohudhuria walimpigia makofi wakati akitoka uwanjani.
Hili linakuwa pigo kubwa kwa Serena anayepambana kuvunja rekodi ya kuwa mchezaji wa tenisi wa kike mwenye mataji mengi zaidi, ambapo mara kwa mara jaribio lake la kutwaa taji la 20 limekuwa likishindikana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Serena aliwashukuru mashabiki zake waliokuwa wakimtia moyo kwa sapoti yao.