Site icon Sports Leo

Simba Sc Yahamia Kwa Sowah

Klabu ya Simba Sc sasa imehamia kwa Jonathan Sowah ikitaka kumsajili baada ya kupata ofa kadhaa za kumuuza Lionel Ateba anayehitajika nchi za kaskazini mwa bara la Afrika.

Awali Sowah alihitajika na Yanga sc lakini mabosi wa klabu hiyo ni kama wamerudi nyuma kumalizia dili hilo wakihofia kuhusu nidhamu ya mshambuliaji huyo mkali wa kufunga mabao ligi kuu ya Nbc nchini.

Mabosi wa Simba Sc wamefungua mazungumzo na Singida Black Stars kuhusu kumsajili mshambuliaji huyo na kama wakifanikiwa basi watamuuza Lionel Ateba kutokana na ofa nono waliyokuwa nayo.

Sowah ni aina ya mshambuliaji mwenye nguvu akiwa na kiwango kikubwa cha kufunga mabao ambapo ameonyesha hilo tangu ajiunge ligi kuu katikati ya msimu huu ulioisha lakini alifanikiwa kuwa katika orodha ya vinara wa mabao nchini.

Tayari makubaliano binafsi baina ya Sowah na Simba sc yamefanyika na kukamilika huku kikwazo kikubwa kikibaki kwa mabosi wa Singida Black Stars kukamilisha mazungumzo hayo na Simba sc kuhusu dau la kuvunjia mkataba wake klabuni hapo.

Exit mobile version