Klabu ya Simba sc imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambulia wa klabu ya Zanaco Fc Moses Phiri raia wa Zambia kwa mkataba wa miaka miwili ambapo hivi sasa inasubiri kumtambulisha tu baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.
Klabu hiyo mabingwa wa ligi kuu nchini mara 18 ilifanikiwa kumsainisha mkataba wa awali staa huyo tangu mwezi wa nne mwaka huu na sasa tayari imemsainisha mkataba wa miaka miwili ikisubiri amalize mkataba wake na klabu ya Zanaco Fc ili imsajili moja kwa moja ambapo atakuja kuchukua nafasi ya Chriss Mugalu ambaye anatemwa akimaliza mkataba wake msimu huu.
Mshambuliaji huyo pia alikua anatakiwa na klabu ya Yanga sc ambapo mmoja wa mabosi wa juu wa klabu hiyo alikwenda mpaka nchini Zambia kufanya mazungumzo na mchezaji huyo lakini hawakufikia muafaka na sasa anatua kwa wapinzani wao Simba sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.