Sports Leo

Simba Sc Yatolewa Crdb Cup

Klabu ya Simba Sc imekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Singida Black Stars katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb nchini.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo mjini Babati ilishuhudia mtanange mkali baina ya timu hizo uliomalizika kwa Simba sc kukubali mabao hayo yaliyowaduwaza mashabiki wa timu hiyo waliofurika uwanjani.

Kocha Fadlu Davis hakua na jinsi zaidi wa kuwapumzisha baadhi wa mastaa wa klabu hiyo ambao walikua na majeraha sambamba na uchovu ambapo alimuanzisha Valentino Nouma na Davis Kameta badala ya Shomari Kapombe na Mohammed Hussein.

Jonathan Sowah alianza kuiandikia Singida Black Stars bao la kwanza dakika ya 16 ya mchezo akitumia uzembe wa mabeki wa kati wa Simba Sc walioshindwa kumkaba na kupiga shuti lililomshinda kipa Moussa Camara.

Dakika ya 34 ya mchezo huo makosa ya kipa Ally Salim aliyeingia kuchukua nafasi ya kipa Moussa Camara aliyeumia baada ya kugongana na Sowah ambapo kipa huyo alihlshindwa kumiliki mpira na kumpasia Emmanuel Keyekeh aliyefunga bao la pili kwa Black Stars.

Mapema kipindi cha pili tena kipa Ally Salim alishindwa kujipanga vizuri katika faulo iliyopigwa na Keyekeh na kuzama moja kwa moja nyavuni na kuipatia Singida Black Stars bao la tatu na kuwamaliza nguvu Simba Sc.

Hata hivyo dakika ya 49 ya mchezo Jean Charles Ahoua alifunga bao zuri la kufutia machozi kwa Simba sc kwa faulo iliyojaa moja kwa moja wavuni.

Dakika tisini za mwamuzi Ahmed Arajiga zilimalizika kwa Black Stars kufanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo ambapo watakutana na Yanga sc katika mchezo wa fainali mwezi huu.

Exit mobile version