Home Makala Simba sc Yawagomea USGN

Simba sc Yawagomea USGN

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kupata alama moja katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Us Gendamarie ya nchini Niger katika mchezo wa kombe la shirikisho uliofanyika nchini humo katika uwanja wa General Seyni Kountche.

Us Gendamarie walikua wa kwanza kupata goli kupitia kwa Wilfred Gbeuli aliapata bao la mapema dakika ya 11 ya mchezo kutokana na uzembe wa mabeki ws klabu ya Simba sc walioshondwa kuondoa hatari langoni mwao.

Mpaka mapumziko Simba sc walikua nyuma kwa bao hilo moja huku ikiwa imelenga shuti mara moja katika ya mashuti matano waliyoyapiga.

banner

Kipindi cha pili dakika za mwanzoni iliwalazimu Us Gendamarie kurudi nyuma kuzuia zaidi mpaka pale walipoweza kumiliki mpira huku wakikosa nafasi kadhaa za kufunga.

Mabadiliko ya kuwaingiza John Boko na Benard Morrison yaliwapa uhai Simba sc na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 83 na kufanya ubao kusomeka 1-1 mpaka dakika ya 90 ya mchezo.

Simba sc sasa ipo juu ya msimamo wa kundi D ikiwa na alama nne katika michezo miwili ya kundi hilo ikishinda dhidi ya Asec Mimosa na kutoa sare dhidi ya Gendamarie

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited