Home Makala Simba Yaitisha Fc Platnum

Simba Yaitisha Fc Platnum

by Sports Leo
0 comments

Ushindi uliopata klabu ya Simba sc dhidi ya Ihefu Fc umeitisha klabu ya Fc Platnum inayotarajiwa kukutana nayo Januari 6 mwakani katika mchezo wa mtoano awamu ya pili utakaofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa awali Fc Platnum wakiwa nyumbani walionekana kuumudu mchezo kiasi cha kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Perfect Chikwende lakini tangu Simba sc irudi nyumbani imekua na matokeo ya ushindi wa mabao mengi ikitandika majimaji Fc 5-0 na Ihefu 4-0.

Fc Platnum imetishika na ushindi huo hasa ikizingatiwa wanakwenda kukutana na Simba sc katika uwanja ule ule walioshinda mabao nane katika mechi mbili hivyo wanalazimika kucheza kwa tahadhari huku wakiongeza umakini katika maandalizi kuelekea mchezo huo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited