Mshambuliaji wa Yanga,Yacouba Sogne amewasili Tanzania leo akitokea nchini Burkina Faso ili kuungana na wachezaji wenzake kambini kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.
Sogne amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Yanga Sc katika msimu wa 2020/2021.
Mchezo wa ufunguzi wa Yanga ligi kuu bara utakuwa dhidi ya Tanzania Prisons Septemba 6 uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.