Mshambuliaji Jonathan Sowah amezidi kuineemesha klabu yake ya Singida Black Stars baada ya jana kufunga bao katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Fountain Gate Fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo mjini Babati.
Sowah alifunga bao la kwanza dakika ya 30 akitumia ufundi mkubwa na kuwazidi maarifa mabeki wa Fountain Gate Fc baada ya kupokea pasi nzuri ya Arthur Badda.
Mabao mengine ya Singida Black Stars yalifungwa na Frank Assink dakika ya 56 pamoja na Emmanuel Keyeke dakika ya 70 kwa faulo kali.
Sowah sasa amefikisha mabao nane ya ligi kuu katika michezo nane msimu huu ambao amejiunga na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu.
Katika msimamo wa wafungaji bora wa ligi kuu nchini mpaka sasa Jean Charles Ahoua anaongoza akiwa na mabao 12 huku Prince Dube akifuatia aliwa na mabao 11 pamoja na Clement Mzize.