Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kwanza wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) baada ya kufungwa mabao 2-0.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa suluhu hukiu Stars ikijitahidi kuonyesha ubabe kwa kushambulia japo haikupata bao licha ya kulaimisha mashambulizi.
Kipindi cha pili Stars ilikata upepo na kusababisha mabao mawili huku makosa ya Shomari Kapombe yakisababisha bao la kwanza dakika ya 61 baada ya kuunawa mpira ndani ya boksi na mwamuzi kuipa penati Zambia iliyofungwa na Collins Sikombe dakika ya 64.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Uzembe wa mabeki wa Stars ulisababisha Zambia kupata bao la pili dakika ya 81 mfungaji akiwa Emmanuel Chabula aliyeunganisha krosi kwa shuti kali na kufanya dakika tisini kumalizika kwa stars kupoteza alama tatu muhimu.