Kocha mkuu wa klabu ya Simba sc Sven Vandebroek amejiuzuru kufundisha klabu hiyo na kuondoka nchini mara moja akielekea nyumbani kwake nchini Ubeligiji.
Taarifa za awali zilidai kwamba kocha huyo alivunja mkataba wake akidai kuwa na matatizo ya kifamilia lakini taarifa rasmi kutoka klabuni hapo zinasema kuwa makubaliano ya pande zote yalifikiwa katika kuvunja mkataba na kocha huyo.
Taarifa hiyo imeonekana kuwastua wadau wa soka nchini hasa ikizingatiwa kuwa imekuja siku moja tu baada ya timu hiyo kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.