Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) limeingia mkataba na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) wa matangazo ya ligi kuu bara kwa njia ya redio kwa miaka kumi wenye thamani ya milioni 3.4.
TBC imeshinda zabuni hiyo baada ya kuzishinda redio nyingine zilizokuwa zinawania kurusha matangazo hayo.
Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa wamewakabidhi TBC matangazo hayo kutokana na uzoefu wao wa miaka mingi na kuwa wao TBC ndiyo wenye haki ya matangazon hayo kwasasa hivyo vituo vingine vya redio vinavyotamani kurusha matangazo kwa njia ya hiyo vionane moja kwa moja na TBC katika kushirikiana kurusha matangazo hayo.