Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(Tcra) imeifungia Televisheni ya Wasafi Tv kwa muda wa miezi sita kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji kwa kuonyesha picha za maudhui yasiyofaa kupitia kipindi cha Tumewasha Live Concert.
Katika barua iliyotolewa na Mamlaka hiyo imeonyesha kwamba Televisheni hiyo iliruhusu msanii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufanya show huku akiwa amevaa mavazi yanayodharirisha utu wa mwanamke.
Televisheni hiyo imefungiwa kuanzia leo huku ikitakiwa kuitumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wa Tv hiyo.