Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza tenda ya kurusha matangazo ya mechi ya ngao ya hisni kati ya Simba na Yanga kwa njia ya redio na televisheni.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Septemba 2021 uwanja wa Benjemin Mkapa jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na TFF kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo mwisho wa kuwasilisha maobi ni tarehe 31 Agosti 2021 saa nne asubuhi.