Klabu ya soka ya Azam Fc leo hii wamemtambulisha Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Dokta Jonas Tiboroha kuwa mkuugenzi mpya wa mpira wa klabu hiyo.
Tiboroha ametambulishwa na Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Abdulkarim Nurdin Popat kushika wazifa huo mbele ya waandishi wa habari.
Mkurugenzi huyo mpya atakuwa na kazi ya kuboresha idara na muundo mzima wa mpira wa miguu wa Azam Fc kuanzia timu za vijana,wakubwa,benchi la ufundi pamoja na maswala yote ya usajili.