Mchezaji wa Tottenham Christian Eriksen agomewa kuuzwa na uongozi wake katika timu ya Inter Milan kwa dau la pauni milioni 10 ambalo liliwekwa mezani na mabosi hao ili kupata saini ya mchezaji huyo.
Christian Eriksen mkataba wake unakaribia kufikia ukingoni lakini mabosi wa Tottenham hawajapata presha kwani wamekomaa na wanahitaji mara mbili ya dau hilo yaani pauni milioni 20 ndipo Inter Milan wafikiriwe kumpata nyota huyo.
Kocha wa Tottenham Jose Morurinho amesema kuwa endapo mchezaji huyo ataachiwa na kuwa mchezaji huru Eriksen alishawahi kumuambia matamanio yake ni kucheza ndani ya Real Madril na Barcelona hivyo lengo lake litakamilika kwani anajiamini kuwa ni mchezaji bora.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.