Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania Stiven Mguto ameomba radhi wadau wa soka kwa kitendo cha kuisahau timu ya Yanga katika upangaji ratiba wa michezo ya ligi kuu wiki hii.
Timu zingine zimecheza katikati mwa wiki huku Yanga ikiachwa wakati ina viporo vingi kuliko timu zingine.
“Ukikosea unasema nini? Samahani! Basi tunaomba tusamehewe kama binadamu tunakosea, lakini wakitaka kutumia kama fimbo kutuadhibu sawa”alisema Mguto.