Klabu ya Chelsea imemuajiri kocha wa zamani wa klabu ya Paris st.German Thomas Tuchel kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Frank Lampard aliyetimuliwa klabuni hapo siku ya januari 25.
Tuchel alitimuliwa na Psg na nafasi yake kuzibwa na Mauricio Pochetino amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka zaidi kuifundisha timu hiyo inayoshika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.
“Ninafurahi kuwa hapa na nina amini nitaonyesha ushirikiano ndani ya timu, pia ninaheshimu ambacho amekifanya Lampard kwa kuwa amefanya jambo kubwa na kazi yake ni nzuri,” .Alisema Tuchel
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.