Home Makala Ufunguzi Chan Kufanyika B/Mkapa

Ufunguzi Chan Kufanyika B/Mkapa

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limeutangaza uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam Tanzania kuwa mwenyeji wa mchezo wa ufunguzi wa Fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN2024) itakayofanyika Kenya, Tanzania na Uganda kuanzia Agosti 2, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Caf ni kuwa uwanja huo utatumika kwa michezo ya Kundi B lenye timu za Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, na Central African Republic.

Ufunguzi  wa michuano hiyo unatarajiwa kufanyika nchini katika uwanja huo siku ya Agosti 2 2025 ambapo kundi B la michuano hiyo itachezwa katika uwanja huo.

banner

Uwanja wa Mkapa siku za karibuni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekua na utaratibu wa kuufanyia marekebisho makubwa ili uweze kukidhi michuano hiyo ambapo pia utatumika katika michuano ya Afcon mwaka 2027.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited