Kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskajaer amesema kuwa yupo kwenye harakati za kumtafuta mbadala wa Marcus Rashford kwa mkopo baada ya kuthibitishiwa na madaktari kuwa hataweza kuwa ndani ya uwanja takribani miezi mitatu.
Rashford ambaye ni majeruhi kwa sasa amekosa mchezo wa jana dhidi ya Liverpool ambao waliwapa kichapo timu yake ya Manchester United cha mabao 2-0 na kuifanya ibaki nafasi ya 5 ikiwa na pointi 34 kibindoni.
“Ni lazima tuangalie namna gani tunaweza kumpata mchezaji ambaye tutampa dili hata la mda mfupi kwa ajili ya kuwa nasi katika msimu huu wa ligi kuu unaoendelea”alisema Solskajaer
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Aliongeza kwa kusema kuwa ni bahati mbaya sana kwa timu ya United kwa sasa kwani ina majeruhi wengi ambao ni wa muhimu kwenye ligi ikiwa ni Marcus Rashford,Anton(martial),Paul(Pogba),Scott(mc Tominay).