Manchester United imekamilisha dili la kumpata Odion Ighalo kwa mkopo wa pauni milioni tatu ingawa dili la United kumnunua jumla halijakamika.
Odion Ighalo anakuwa mbadala wa Marcus Rashford ambaye ndiye kinara wa United akiwa na mabao 14 ila kwa sasa anasumbuliwa na majeruhi ambayo yatampelekea kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita.
Vita kubwa wamepata United kuwania saini ya mchezaji huyo kwani Jose Mourinho wa Spurs naye alikuwa anamuhitaji Ighalo kabla dirisha la mwezi Januari halijafugwa.
Nyota huyoanatarajiwa kutua United mwishoni mwa msimu huu akiwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer ambaye amesema kuwa Odion ni mchezaji mwenye uzoefu na uwezo ndani ya Uwanja.
Nyota huyo raia wa Nigeria, mwenye miaka 30 amefunga jumla ya mabao 46 kwenye mechi 72 alizocheza akiwa na Shanghai Shenhua.