Site icon Sports Leo

Usajili Wote Yanga Sc 2025-2026

Klabu ya Yanga SC imeingia kwa kishindo kwenye dirisha la usajili wa msimu wa 2025/2026 na kuonyesha dhamira ya kweli ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC huku ikilenga pia kufanya mambo makubwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wanajangwani hawa wamesajili nyota wapya wenye majina makubwa na wengine chipukizi, wote wakitarajiwa kuongeza nguvu mpya na ushindani ndani ya kikosi cha kocha Roman Folz.

MIKWARA YA MASTAA WAPYA

Katika usajili huu, Yanga imehakikisha haichukui majina tu bali wachezaji wenye ubora unaoendana na kasi ya mpira wa kisasa. Kila mmoja amesajiliwa kwa mkakati maalum wa kuongeza kitu tofauti, kuanzia ulinzi, kiungo hadi safu ya ushambuliaji.

1. FRANK ASSINK– Beki wa Kati (Ivory coast)
Beki huyu wa Ivory Coast mwenye umbo la kisiki ni nguzo mpya ya safu ya ulinzi. Ameshacheza soka la kiwango cha juu hapa Tanzania katika klabu ya Singida Black Stars na anajulikana kwa uwezo wa kuzuia washambuliaji wa kasi na kutumia mwili wake vizuri kwenye mipira ya juu. Kwa usajili wake, mashabiki wa Yanga wana uhakika safu ya ulinzi haitakuwa na mianya kama ilivyokuwa msimu uliopita.

2. OFFEN CHIKOLA “Messi wa Morogoro” – Winga (Tanzania)
Huyu ni kijana aliyeibuliwa kutoka Tabora United na ni moja ya winga wenye kasi zaidi kwenye Ligi ya NBC. Yanga imemleta ili kuongeza mbio na chachu ya ushambulizi. Mashabiki wanatarajia kuona krosi zake za moto zikimiminwa kwa washambuliaji ndani ya boksi. Bila shaka ataongeza ushindani mkubwa kwenye nafasi ya winga ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitegemewa na Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli.

3. Celestine Ecua – Kiungo Mshambuliaji (Chad)
Huyu ni staa wa Chad  mwenye miguu laini na akili kubwa ya mpira. Yanga imemsajili ili kuwa “mchora ramani” wa mashambulizi. Ana uwezo wa kupenyeza mipira ya hatari na kutoa pasi za mwisho (assist) kwa washambuliaji. Katika michuano ya CAF, Yanga itamhitaji kama silaha ya kutengeneza nafasi mbele ya mabeki wagumu wa Afrika Kaskazini.

Eccua aliyetokea katika klabu ya Assec Mimosas ya nchini Ivory coast ambako aliibuka kuwa mchezaji bora na mfungaji bora wa ligi hiyo ambapo msimu huu ameamua kuichezea timu ya Taifa ya Chad badala ya Ivory Coast.

4. Balla Moussa Conte-(Guinea)
Yanga hawajacheza mchezo kwenye safu ya ulinzi. Wameleta kiungo huyu wa Guinea mwenye uzoefu wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Conte anajulikana kwa reflex kali na ujasiri wa kusimama katika eneo la kiungo cha ukabaji hata mbele ya washambuliaji wakali na kuwadhibiti kwa usahihi.

Usajili wake unamaanisha kutakuwa na ushindani mkubwa kwa eneo la kiungo akichuana na Mudathir Yahaya na Duke Abuya.

5. Andy Boyeli – Straika (Zambia)
Kwa mashabiki wa Yanga, jina hili litakuwa gumzo msimu mzima. Boyeli ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kumalizia nafasi. Ni aina ya mshambuliaji anayependa kukimbia nyuma ya mabeki na kutumia mwili wake kushindana. Anatarajiwa kuwa mfungaji wa mabao mengi na kuchukua nafasi kubwa kwenye kampeni ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

NDOTO YA AFRIKA

Kwa kusajili mastaa hawa, Yanga SC imeonyesha wazi kuwa haitaki kubaki historia ya kufika fainali ya Kombe la Shirikisho pekee. Lengo ni moja – kuibuka vinara wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Kocha Gamondi ana kikosi kipana, chenye mchanganyiko wa uzoefu na damu changa.

Assink na Conte wataimarisha ulinzi, Eccue atakuwa kiungo tegemeo, huku Chikola akiongeza kasi pembeni na Boyeli akimalizia kazi. Hii ni formula inayoweza kuipatia Yanga mchanganyiko hatari zaidi kuliko misimu iliyopita.

LIGI KUU NBC – VITA YA DAR

Ndani ya Ligi Kuu, usajili huu utaiweka Yanga katika nafasi ya juu ya kupigania ubingwa dhidi ya watani wa jadi, Simba SC. Mashabiki tayari wanahesabu siku kuelekea mchezo wa kwanza wa Kariakoo Derby. Wengi wanasema Simba safari hii itakuwa na kibarua kigumu zaidi, maana Yanga imejipanga kisayansi na kimkakati.

HITIMISHO

Kwa mashabiki wa Yanga, msimu wa 2025/2026 unatarajiwa kuwa wa burudani ya hali ya juu. Usajili wa nyota wapya umeleta ari mpya, matumaini na hamasa ya kupigania mataji makubwa. Wananchi wanataka kuona jezi ya kijani na njano ikitikisa si tu Tanzania bali bara zima la Afrika.

Wanajangwani sasa wanasema kwa sauti moja: “Huu ndiyo msimu wa kuandika historia mpya!”

Exit mobile version