Home Makala Utaratibu Wa Ligi Kuu Ujerumani Upo Hivi

Utaratibu Wa Ligi Kuu Ujerumani Upo Hivi

by Dennis Msotwa
0 comments

Waendeshaji wa Bundesliga (DFL) wamepania kutumia mbinu zote zitakazowawezesha wadau wa soka kufanikisha mipango ya kukamilisha kampeni za msimu huu licha ya kwamba janga la virusi vya homa kali ya corona halijadhibitiwa vilivyo .

Kutotema mate ni moja ya mapendekezo ambayo viongozi wa ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) wamesisitiza katika mwongozo kwa wanasoka wa kipute hicho kinachotarajiwa kurejelewa wikiendi ya Mei 16, 2020.

Siku ya mechi maafisa wa afya wa vikosi husika watahitajika kuwasilisha fomu kwa viongozi wa DFL kuthibitisha kuwa wanasoka wote wamefanyiwa vipimo vya virusi vya Corona na iwapo ripoti hiyo haitawasilishwa kufikia saa nne na nusu asubuhi, basi pendekezo la kufutiliwa mbali kwa mechi litatolewa.

banner

Wanasoka wanaochezea nyumbani wanatakiwa kuwasili uwanjani kwa magari yao binafsi, kila mmoja akijiendesha huku vikosi vya kigeni vitatakiwa kusafiri kwa kutumia idadi kubwa ya mabasi ili kuhakikisha umbali wa mita moja na nusu kati ya wachezaji unadumishwa.

Vyumba vingi vitawekwa kwenye kila uwanja ili wachezaji watumie kubadilishia nguo ikiwa ni juhudi za kuhakikisha kwamba hawakaribiani,pia vyumba hivyo vitanyunyiziwa dawa za kuua virusi mara kwa mara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited